Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 151 Zamani Watoto Waliletwa Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 151 Zamani Watoto Waliletwa Maneno ya wimbo

 

Zamani watoto waliletwa kwa Yesu,
Wanafunzi walitaka kuwafukuza,
Kabla hawajaondoka akawaita haraka,
Watoto wadogo na waje kwangu.

Nitawakubali, nami nitawalea,

Ni mchunga wao hawa, msiwafukuze;

Wakinipenda mioyoni, na waje kwangu mbinguni.

Watoto wadogo na waje kwangu.

Ndiye Bwana mwema, huwaita watoto,

Lakini wako wengi wasiomjua,

Hawajui Chuo chake, wala lile neno lake,

Watoto wadogo na waje kwangu.

Na kila kabila ya watu duniani,

Waje kwa Yesu, watupe sanamu zao;

Ewe mungu wa Mapenzi, wapeleke wakufunzi,

Wakafunze wote, wafike kwako.

Exit mobile version