Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 145 Baba Yetu Aliye Mbinguni Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 145 Baba Yetu Aliye Mbinguni Maneno ya wimbo

 

Baba yetu aliye mbinguni,
Amenifurahisha yakini
Kuniamba mwake chuoni
Ya kuwa nami Yesu pendoni.

Anipenda mwokozi Yesu,
Anipenda, Anipenda:
Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda mimi.

Nimuachapo kutanga mbali Yeye Yu vivyo, hupenda kweli,
Hunirejeza Kwake moyoni:
Kweli yu nami Yesu pendoni.

Anipenda!
Nami nampenda;
Kwa Wokovu alionitenda:
Akanifia Msalabani
Kwa kuwa nami Yesu Pendoni.

Haya kujua yanipa raha;
Kumuamini kuna furaha:
Kumfukuza mara Shetani,
Kwona yu nami Yesu pendoni.

Sifa ni nyingi asifiwazo,
Moja ni sana katika hizo,
Wala siachi hata mbinguni,
Kwimba Yu nami Yesu pandoni.

Exit mobile version