Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 143 Wakati Wa Baraka Karibu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 143 Wakati Wa Baraka Karibu Maneno ya wimbo

 

Wakati wa baraka u karibu,
Utakua mchana au usiku;
Arusi ya bibi pamoja na Bwana,
Mfalme wetu tutamwona.

Na tutamwona, na tutamwona,
Mfalme wetu tutamwona;
Yuaja tena tutamkaribisha,
Mfalme wetu tutamwona.

U tayari leo akikuita?
Atafurahi nawe kabisa?
Mbinguni ni kwake, na kwa watu wake,
Mfalme wetu tutamwona.

Ndugu yangu, uwe tayari kwake,
Kumvika taji kichwani pake;
Falme za dunia na wainamishwe,
Mfalme wetu tutamwona.

Exit mobile version