Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 141 Yesu Yuaja Na Utukufu Wake Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 141 Yesu Yuaja Na Utukufu Wake Maneno ya wimbo

 

Yesu yuaja, na utukufu wake,
Kuwapokea waaminifu wake;
Labda atakuja hapo asubuhi
Wakati wa pambazuko.

Bwana Yesu, lini, lini,
Tutakapoimba? Kristo yupo, Aleluya!
Aliye Amin, Aleluya Amin!
Yesu atakuja labda adhuhuri,
Labda ataonekana magharibi;
Ama katika usiku wa manane,
Pamoja na utukufu.

Watu wakimwimbia Yesu, Hozana,
Pamoja na malaika wake Bwana;
Kwa neema yake atatupokea,
Yesu atakaporudi.

Furaha nyingi!
tutaishi mbinguni,
Hakuna ugonjwa wala kufariki;
Hatutakuwa na hofu duniani,
Yesu atakaporudi.

Exit mobile version