Nyimbo za wokovu
Wimbo 140 Siku Hizi Ni Za Mwisho Maneno ya wimbo
Siku hizi ni za mwisho,
Tumaini letu hiyo;
Kwamba Yesu yu karibu,
Bwana wa mabwana ndiye Huyu.
Yu karibu, Yu karibu,
Kwa mema tutamkaribisha;
Asubuhi au labda jioni,
Twajua ndiye karibu.
Kwa dalili duniani,
Tena zile za hewani;
Hayo yahubirieni,
Ya kwamba Yesu yuaja tena.
Wafu waliomo Kristo,
Wafufushwe na uwezo;
Atakaporudi Kristo,
Ataweka tayari makao.
Na sisi tuliobaki,
Tutanyakuliwa kweli;
Si bure kutumaini,
Farijiane na neno hili.