Nyimbo za wokovu
Wimbo 135 Nitwae Hivyo Nilivyo Maneno ya wimbo
Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu, naja.
Hivi nilivyo;
si langu Kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu naja.
Hivi nilivyo;
sioni Kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu, naja.
Hivi nilivyo kipofu,
Maskini na mpungufu;
Wewe u mtimilifu,
Bwana Yesu, naja.
Nawe hivi utanitwaa;
Nisisubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa Bwana Yesu, naja.
Hivi nilivyo mapenzi,
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu, naja.