Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 119 Muda Mwingi Nilipotea Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 119 Muda Mwingi Nilipotea Maneno ya wimbo

 

Muda mwingi nilipotea,
Sikufahamu Msalaba;
Wala aliyenifilia,
Kwa Kalvari.

Rehema bure na Neema.

Samaha nalo nilipewa;
Ndipo aliponifungua,
Kwa Kalvari.

Kwa Neno lake Bwana Mungu,
Nilijiona mimi mwovu;
Nikageuka na kutubu,
Kwa Kalvari.

Yote kwa Yesu namtolea,
Ndiye mfalme wa pekee Sasa;
Kwa furaha nitamwimbia,
Kwa Kalvari.

Jinsi pendo lilivyo kuu,
Neema ilishushwa toka juu,
Alitufanyia wokovu,
Kwa Kalvari.

Exit mobile version