Nyimbo za wokovu
Wimbo 118 Aliteswa, Aliteswa Maneno ya wimbo
Aliteswa, aliteswa,
Msalabani Yesu aliteswa;
Dhambi zangu ameziondoa,
Mahali pangu aliteswa.
Alikufa, alikufa,
Msalabani Yesu alikufa;
Kwa kifo chake nakombolewa,
Kwa kuwa Yesu alinifia.
`Kafufuka,
`Kafufuka,
Kaburini Yesu alitoka;
Nami nimewekwa huru pia,
Kwa kuwa Yesu alifufuka.
Yuko hai, yuko hai,
Mbinguni anaishi Mwombezi;
Daima huniombea mimi,
Kwa Yesu adumu hai.
Atarudi, atarudi,
Siku moja Yesu atarudi;
Na tumwonapo tutafurahi,
Kwa kupelekwa kwake mbinguni.
Sifa kwake, sifa kwake,
Mbinguni na huimbwa milele;
Kwa furaha, masifu, na shangwe,
Tutamwimbia Yesu milele.