Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 116 Uwe Huru Kutoka Dhambini Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 116 Uwe Huru Kutoka Dhambini Maneno ya wimbo

 

Uwe huru kutoka dhambini,
Uko uwezo wa ajabu;
Juu ya uovu uwe mshindi,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Uwezo wa ajabu ndimo
Damuni mwa Yesu,
Uwezo wa ajabu ndimo
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Uwe huru juu tamani yako,
Uko uwezo wa ajabu;
Njoo, utakaswe katika mto,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Uwe mwenye moyo safi mno,
Uko uwezo wa ajabu;
Alama itoke kwa uwezo,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Ufanye kazi kwa Mfalme Yesu,
Uko uwezo wa ajabu;
Uishi daima kumsifu,
Damuni mwa Mwana-Kondoo.

Exit mobile version