Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 112 Yesu Ni Jina Nipendalo Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 112 Yesu Ni Jina Nipendalo Maneno ya wimbo

 

Yesu ni jina napendalo,
Napenda kulisikia;
Napenda kulitamka hilo,
Lililoniridhisha.

Yesu, nakupenda,
Yesu, nakupenda;
Yesu, nakupenda,
Kwani ulinipenda.

Jina hilo huniambia,
Mwokozi alinipenda;
Damu yake ilimwagika,
Nipate kuokoka.

Lanionyesha sifa yake,
Iliyo katika Baba;
Njia ijapokuwa giza,
Yesu huniongoza.

Lanidhihirishia Yesu,
Aliyenihurumia;
Laondoa taabu yangu,
Niwe wake daima.

Exit mobile version