Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 111 Damu Imebubujika Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 111 Damu Imebubujika Maneno ya wimbo

 

Damu imebubujika,
Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka
Husafiwa kweli (3)

Ilimpa kushukuru
Mwivi mautini;
Nami nisiwe udhuru,
Yanisafi ndani. 3)

Kondoo wa kuuawa,
Damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa Kwa utimilivu. (3)

Bwana, tangu damu yako Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako;
Taimba milele. (3)

Nikifa tazidi kwimba Sifa za wokovu,
Ulimi ujaponyamaa Vumbini mwa ufu. (3)

Bwana, umenikirimu Nisiyestahili Kwa damu yako sehemu Ya mali ya kweli. 3)

Nikubali kukwimbia,
Mbinguni milele
Mungu nitakusifia
Jina lako pweke. (3)

Exit mobile version