Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 109 Peleka Jina La Yesu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 109 Peleka Jina La Yesu Maneno ya wimbo

 

Peleka jina la Yesu
Ko kote uendako;
Litafurahisha moyo,
Peleka uendako.

Thamani, na tamu,
Ni jina lake Yesu;
Thamani, na tamu,
Ni jina lake Yesu.

Peleka jina la Yesu Liwe silaha zako;
Utakapojaribiwa,
Lilia jina hilo.

Yesu, jina la thamani,
Limenifurahisha;
Nikiwasili Mbinguni,
Atanikaribisha.

Kwa jina la Bwana Yesu,
Nimejiinamisha;
Ndiye Mfalme wa wafalme,
Katika ya maisha

Exit mobile version