Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 108 Yesu Awakubali Wakosa Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 108 Yesu Awakubali Wakosa Maneno ya wimbo

 

Yesu awakubali,
Wakosa, wahalifu,
Wambieni wa mbali
Habari ya wokovu.

Tangazeni kwa bidii
Akubali wakosa!
Liwe neno dhahiri
Akubali wakosa!
Awakubali Bwana
Neno lake amini,
Watu kila aina,
Waje kwake tengoni.

Mimi ni safi moyo
Na mbele ya sheria,
Aliyesafi roho
Kwake ilitimia.

Akubali wakosa:
Nami anikubali:
Alivyonitakasa
Mbinguni niwasili.

Exit mobile version