Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 105 Siku Ya Mbingu Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 105 Siku Ya Mbingu Maneno ya wimbo

 

Siku ya mbingu kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.

Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.

Na siku moja walikwenda naye
Wakamkaza Msalabani;
Aliumia, aliaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.

Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini, alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni Mwokozi, kwake kwa twaokoka.

Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka, kwa kushinda kwake,
Naye yuko milele mbinguni.

Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi wangu, tutaonana.

Exit mobile version