Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 10 Yesu, Nikikumbuka Maneno ya wimbo

Nyimbo za wokovu

Wimbo 10 Yesu, Nikikumbuka Maneno ya wimbo

 

Yesu, nikikumbuka
Hwona tamu moyo,
Itazidi nikikwona,
Uso ukaapo.

Hakuna kamwe tamko,
Lenye kusemeka,
Tamu kama jina hilo,
wala kuwazika.

Jinsi ilivyo hakuna,
Tangu kale kitu
Cha kuzidi lako jina
Mwokozi wa watu.

Tumai ya watubuo,
Nyemi za wapole,
Wa kwomba, watafutao,
Wabariki wale.

Ulivyo kwa wakwonao
Havijulikani,
Pendo zako wajuao
Ndio wa pendoni.

Yesu huku U raha kuu,
U ujira kule:
Ni wewe letu shangwe tu,
Milele, milele.

Exit mobile version