Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 98 Twasoma ni Njema Sana. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 98 Twasoma ni Njema Sana. Maneno ya wimbo

 

Twasoma, ni njema sana
Mbinguni kwa Bwana
Kwa Bwana, dhambi hapana
Mbinguni, kwa Bwana
Malaika wema wako
Vinanda vizuri viko
Na majumba tele yako
Mbinguni kwa Bwana

Siku zote ni mchana
Ni nchi ya raha
Wala machozi hapana
Ni nchi ya raha
Walioko wauona
Uso wa Mwokozi, tena
Jua jingine hapana
Ni nchi ya raha

Nyama na vita viovu
Havimo kabisa
Kifo nacho, na ubovu
Havimo kabisa
Ni watakatifu wore
Wameoshwa dhambi zote
Wasiosafiwa wote
Hawamo kabisa

Tuna dhambi pia sote
Mwokozi akafa
Kwake tutaoshwa zote
Mwokozi akafa
Kwake twapata zote
Tutawona utukufu
Mbinguni tutamsifu
Mwokozi akafa

Baba, mama, ndugu zetu
Twendeni kwa Bwana
Huku chini iko kwetu
Twendeni kwa Bwana
Tusishikwe na dunia
Na dhambi kutulemea
Tutupe vya chini pia
Twendeni kwa Bwana

Exit mobile version