Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 97 Kaa Nami. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 97 Kaa Nami. Maneno ya wimbo

 

Kaa nami, ni usiku tena
Usiniache gizani, Bwana
Msaada wako haukomi
Nili peke yangu, kaa nami

Siku zetu hazikawi kwisha
Sioni la kunifurahisha
Hakuna ambacho hakikomi
Usiye na mwisho, kaa nami

Nina haja nawe kila saa
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
IlaWewe? Bwana, kaa nami

Sichi neno uwapo karibu
Nipatalo lote, si taabu
Kifo na kaburi haviumi
Nitashinda kwako, kaa nami

Nilalapo nikuone wewe
Gizani mote nimulikiwe
Nuru za mbinguni hazikomi
Siku zangu zote kaa nami

Exit mobile version