Nyimbo Za Sifa
Wimbo 94 Maelfu na Maelfu. Maneno ya wimbo
Maelfu na maelfu
Wenye nguo bora!
Masafu ya waongofu
Wenye na bendera
Amekwisha kamili
Vita vya Shetani
Fungueni Iango hili
Njoni, ingieni!
lmbeni Aleluya
Zipae Mbinguni!
Pigeni sana sauti
Kwa kutumaini!
Kwa hiyo viliumbwa
Nchi hata Mbingu
Dhiki za muda zikisha
Asi?weYesu
Loo! Tukionana
Pwani ya ng’amboni!
Loo! Tukishirikiana
Milele Mbinguni!
Midomo yote pia
Huko itaimba
Wajane kufufukiwa
Na kila yatima!
Himiza enzi yako
Uliyetufia
Utimize watu wako
Wakosaji pia
Mpendwa wa taifa
Twakutumaini!
Uzifunue ishara
Urudi enzini!