Nyimbo Za Sifa
Wimbo 93 Huyo Ndiye! Anashuka. Maneno ya wimbo
Huyo ndiye! anashuka
Aliyetu?lia
Wengi waliookoka
Wakimfurahia
Aleluya!
Yesu aturudia.
Sote tutamtazama
Amekaa Kitini
Nao waliomchoma
Kumkaza Mtini
Na kilio
Wamuone enzini
Alama za kifo chake
Hata sasa anazo
Na waaminifu wake
Wapendezewe nazo
Alipata
Kwetu alama hizo
Wokovu utakiwao
Sasa wapatikana
Na watakatifu hao
Mbinguni wakutana
Kumlaki
Ndiyo siku ya Bwana
Wakusujudie wote
Mbele ya Kiti chako
Zako, Bwana, nguvu zote
ltwae miliki yako
Njoo Bwana