Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 92 Tazameni Huyo Ndiye. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 92 Tazameni Huyo Ndiye. Maneno ya wimbo

 

Tazameni Huyo ndiye
Mwenye kushinda vita
Haya, tumsujudie
Nyara anaziieta
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini

Msifuni malaika
Mtukuzeni sana
Wote waliookoka
Watamsifu Bwana
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini

Walimfanya dhihaka
Zamani wenye shari
Kwao waliookoka
Ni Bwana wa fahari
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini

Nyimbo nzuri, sikizeni
Ni nyimbo za sifa kuu
Za Bwana Yesu Kitini
Kutawazwa,Yeye tu
Watu wote msifuni
Sasa yumo Kitini

Exit mobile version