Nyimbo Za Sifa
Wimbo 91 Tumrudie Bwana. Maneno ya wimbo
Mbona washanga njiani?
Mbona warejea nyuma?
Warudi tena gizani
Alimokuotoa Bwana?
Ni ya bure yote haya
Uliyofunzwa ya Mungu?
Ni bure ameku?a
Bwana Yesu kwa uchungu?
Wamtia Kristo aibu
Na maneno yake pia!
Siku yaja ya hesabu
Utamjibuje Bwana
Upandayo tena hayo
Halafu utayavuna
Rudi kwa Bwana upesi
Mwombe akupokee tena