Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 87 Mapenzi Yako Yafanyike Bwana. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 87 Mapenzi Yako Yafanyike Bwana. Maneno ya wimbo

 

Mapenzi yako yafanyike
Wewe M?nyanzi, nami towe
Uni?nyange upendavyo
Mimi tayari, naja kwako

Mapenzi yako yafanyike
Unihojie dhambi zote
Unisa?she vya kimwili
Niinamapo Msalabani

Mapenzi yako yafanyike
Mimi dhaifu, mimi mnyonge
Uwezo wote, kwako kweli
Sasa niponye, Ee, Mwokozi

Mapenzi yako yafanyike
Natoa kwako vitu vyote
Maisha, mali, moyo, mwili
Vyote ni vyako, kweli, kweli

Mapenzi yako yafanyike
Mapenzi yangu yavunjike
Ninakubali uwe bwana
Ni mali yako, twaa kabisa

Mapenzi yako yafanyike
Unitawale sikuzote
Sura ya Yesu umba kwangu
Nijaze Roho nayo nguvu

Exit mobile version