Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 86 Ndiyo Damu ya Baraka. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 86 Ndiyo Damu ya Baraka. Maneno ya wimbo

 

Ndiyo damu ya baraka, ituoshayo wakosa
Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu
Takuwa safi kabisa

Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa mtini
Na maumivu si haba yaliyompata chini
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa

Sai kabisa; safi kabisa!
Ndicho kinitakasacho
Nami ni sai kabisa

Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijito pako naja naamini sasa
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa

Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu
Takuwa safi kabisa

Exit mobile version