Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 84 Aliteswa, Aliteswa. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 84 Aliteswa, Aliteswa. Maneno ya wimbo

 

Aliteswa, aliteswa
MsalabaniYesu aliteswa
Dhambi zangu ameziondoa
Mahali pangu aliumizwa

Alikufa, alikufa
Msalabani Yesu alikufa
kwa kifo chake nakombolewa
Kwa kuwa Yesu alini?a

Kafufuka, ‘kafufuka
Kaburini Yesu alitoka
Nami nimewekwa huru pia
Kwa kuwaYesu alifufuka

Yuko hai, yuko hai
Mbinguni anaishi Mwombezi
Daima huniombea mimi
kwa kuwaYesu adumu hai

Atarudi, atarudi
Siku mojaYesu atarudi
na tumwonapo tutafurahi
Kwa kupelekwa kwake Mbinguni

Sifa kwake, sifa kwake
Mbinguni na huimbwa mileie
Kwa furaha, masifu, na shangwe
TutamwimbiaYesu milele

Exit mobile version