Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 83 Deni ya Dhambi llimalizika. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 83 Deni ya Dhambi llimalizika. Maneno ya wimbo

 

Deni yangu ya dhambi
Yesu amelipa
Kwake Msalabani
Nilipewa uzima

Deni ya dhambi
Msalabani
Ilimalizikia
Ni huru kabisa

BwanaYesu asema
“Mwanangu dhaifu
Uwezo na ushindi
Hupatikana kwangu

Bwana, kweli naona
Nguvu zako pekee
Huondoa ukoma
Niwe kipya kiumbe

Sina wema moyoni
Nidai neema
Nakubali kabisa
Kwa damu kusafiwa

Hata huko Mbinguni
Miguuni pake
“Yesu alini?a”
Nitaimba milele

Exit mobile version