Nyimbo Za Sifa
Wimbo 80 Kwa Wingi wa Nyama. Maneno ya wimbo
Kwa wingi wa nyama
Na sadaka pia
Hupata wapi salama
Kwondoa hatia?
Sadaka ni Yesu
Hwondoa makosa
Dhabihu mwenye jina kuu
Atanitakasa
Kwa yangu imani
N ikuweke sasa
Mkono mwako kichwani
Kukiri makosa
Roho yakumbuka
Mambo ya Mtini
Mzigo ulijitweke
Ndiyo yangu deni
Deni hutanguka
Tukimuamini
Kwa damu tumeokoka
Twimbe furahani