Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 8 Yesu Kwetu ni Rafiki. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 8 Yesu Kwetu ni Rafiki. Maneno ya wimbo

 

Yesu kwetu ni Rafiki
Hwambiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu
Dua angesikia

Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia.

Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kwendela,
Ujapodhirauliwa
Ujaporushwa pia.
Watu wangekudharau,
Wapendao dunia
Hukwambata mikononi
Dua atasikia

Exit mobile version