Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 75 Msalaba wa Aibu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 75 Msalaba wa Aibu. Maneno ya wimbo

 

Msalaba wa aibu
Ulinipa amani
Uliniondoa kifungoni
Nilimotesekea

Ee, Mwokozi wangu,Yesu
Nitamwendea nani?
Najiweka Msalabani
Nikaoshwe damuni

Nakupenda BwanaYesu
Kwa kunipenda kwako
Napendezwa nikutumikie
Maisha yangu yote

Usifiwe BwanaYesu
Kwa ulivyonifia
Aleluya, nakushukuru
Uliyenikomboa

Msalaba ulishinda
Nguvu zake adui
lli mimi nikombolewe
Niwe mwana wa Mungu

Exit mobile version