Nyimbo Za Sifa
Wimbo 73 Twendeni! Haraka!. Maneno ya wimbo
Twendeni Haraka!Tupeleke Neno
Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza
Bwana alisema nendeni po pote
Kawafundisheni mataifa yote
Pelekeni lnjili kwajina la Yesu
Upesi! Twendeni haraka!
Twendeni Haraka!Tupeleke Neno
La upendo wa Mungu kwa watu wote
Aliyeupenda sana ulimwengu
Akamtoa Yesu mwana wake pekee
Kaleta wokovu, tumtangazeni
Upesi! Twendeni haraka!
Twendeni Haraka!Tupe|eke Neno
La uzima kwa watu waliokufa
Mateka ya Shetani litafungua
Litaponyesha na kuwapa amani
Twendeni upesi, tukawakoe
Upesi! Twendeni haraka!