Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 71 Sioshwi Dhambi Zangu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 71 Sioshwi Dhambi Zangu. Maneno ya wimbo

 

Sioshwi dhambi zangu
Bila damu yake Yesu
Hapendezewi Mungu
Bila damu yake Yesu

Chorus
Hakuna kabisa
Dawa ya makosa
Yo kututakasa
Ila damu yake Yesu

La kunisa? sina
Ila damu yake Yesu
Wala udhuru tena
Ha damu yake Yesu

Sipati patanishwa
Bila damu yake Yesu
Hukumu yanitisha
Bila damu yake Yesu

Sipati tumaini
Bila damu yake Yesu
Wema wala amani
Bila damu yake Yesu

Yashinda ulimwengu
Hiyo damu yake Yesu
Na kutufikisha juu
Hiyo damu yake Yesu

Twaimba: Utukufu
Una damu yake Yesu
Milele twaisifu
Hiyo damu yake Yesu

Exit mobile version