Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 66 Bwana Uliyewaita. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 66 Bwana Uliyewaita. Maneno ya wimbo

 

Bwana uliyewaita
Watakatifu wako
Wawe mitume, wachunga
Walishe kundi Iako

Chorus
Wanyonge na wenye hofu
Wakawa mashujaa
Na wapole wo kunena
Wasiwe kunyamaa

Hata leo wawataka
Watakatifu wako
Nawe wauliza tena
Ni nani aliyeko
Atakaye nimtume
Afundishe vijana?
“Ni tayari, Bwana wangu,
Nitume mimi Bwana.”

Nitume na mimi, Bwana
Kaka ulivyotumwa
Habari ya msamaha
Na dhambi kutubiwa
Niwahubiri wakosa
Na waliopotea
Wokovu u wake Bwana
Aliyewa?lia

Astahiliye hapan
Kutamka habari
Lakini Wewe waweza
Kutufanya tayari
Neno lako tulijue
Tupe na Roho yako
Hayatakuwa ya bure
Haya Maneno yako

Exit mobile version