Nyimbo Za Sifa
Wimbo 55 Naendea Msalaba. Maneno ya wimbo
Naendea Msalaba
Ni mnyonge na mpofu
Yapitayo naacha
Nipone Msalabani
Chorus
Na kutumaini tu
Ewe Mwana wa Mungu
Nainamia kwako
Niponye, Mponye wangu
Nakulilia sana
Nalemewa na dhambi
Pole Yesu asema
“Nitazifuta zote.”
Natoa vyote kwako
Nafasi nazo nguvu
Roho yangu na mwili
Viwe vyako milele
Kwa damu yake sasa
Nimegeuka roho
Nikaziacha tamaa
NimfuateYesu tu
Yesu yuaja tena!
Nimepevuka kwake
Kila chembe kamili
Msifuni Yeye Mponya!