Nyimbo Za Sifa
Wimbo 52 Yesu Nataka Kutakaswa Sana. Maneno ya wimbo
Yesu nataka kutakaswa sana
Nataka moyo uwe enzi yako
Ukiangushe kilichoinuka
Unioshe sasa niwe mweupe
Chorus
Mweupe tu, ndiyo mweupe
Ukiniosha nitakuwa sa?
Bwana Yesu, unitazame sasa
Unifanye niwe dhabihu hai
Najitoa kwako, na moyo wote
Unioshe sasa niwe mweupe
Bwana kwa hiyo nakuomba sana
Nakungojea miguuni pako
Naomba unioshe damuni tu’
Unioshe sasa niwe mweupe
Bwana ninadumu kukungojea
Niumbie moyo safi, Ee Mungu
Wanaokujia hutupi kamwe
Unioshe sasa niwe mweupe