Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 5 Baba, Mwana, Roho. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 5 Baba, Mwana, Roho. Maneno ya wimbo

 

Baba, Mwana, Roho, Mungu
mwenye enzi
Kila tukiamka tunakuabudu
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa
mapenzi,
Ewe utatu, tunakusifu

Baba, Mwana, Roho, wakuaminio
Wanakutolea shukurani zao
Wakusujudia malaika nao
Wewe u mwanzo, nawe u mwisho

Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani
Utukufu wako hauoni kosa
U Mtakatifu, nawe u mapenzi
U peke yako. mwenzio huna

Baba, Mwana, Roho, Mungu
mwenye enzi
Ulivyoviumba vyote vyakusifu
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa
mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu

Exit mobile version