Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 48 Yesu Nakupenda, U Mali Yangu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 48 Yesu Nakupenda, U Mali Yangu. Maneno ya wimbo

 

Yesu nakupenda, U mali yangu
Anasa za dhambi sitaki kwangu
Na Mwokozi aliyeniokoa
Sasa nakupenda, kuzidi pia

Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele
Uhai wako ukanicolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia

Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini
Taji ya miiba aliyoivaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia

Niwapo hai, niwapo maiti
Kupendana nawe kamwe siachi
Hari za kifo zikinienea
Sasa nakupenda, kuzidi pia

Mawanda mazuri na masikani
Nivatazamapo huko Mbinguni
Tasema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia

Exit mobile version