Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 46 Naweka Dhambi Zangu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 46 Naweka Dhambi Zangu. Maneno ya wimbo

 

Naweka dhambi zangu
Juu yake Bwana
Kuziondoa, kwangu
Hulemea sana
Na uaili wangu
Ameuondoa
Dawa yangu ni damu
Kwa hiyo napoa

Na uhitaji wangu
Nitamjuvisha
Kwa upungufu wangu
Yeye anatosha.
Majonzi yangu yote
Na mizigo yangu
Acachukua vyote
Yesu Bwana Wangu

Na roho yangu nayo
Imechoka sana
Namletea hiyo
Ilindwe na Bwana
Ni jema jina lake
Nalo lapendeza
lmanweli na kwake
Tutalitukuza

Natamani daima
Niwe kama Bwana
Mpole, tena mwema
Wa mapenzi sana
Zaidi natamani
Kwenda kwake juu
Nikaone mbinguni
Enzi yake kuu

Exit mobile version