Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 4 Jina LakeYesu Tamu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 4 Jina LakeYesu Tamu. Maneno ya wimbo

 

Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondoiea
Roho iliyoumia
Kwalo hutibika
Chakula, njaani pia
Raha, tukichoka.

Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi
Kwangu ni akiba.

Yesu, Mchunga, Rafiki,
Mwalimu, kuhani
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki
Uzima kifoni.

Moyo wangu hauwezi
Kukusifu kweli
Ila sifa zangu hizi
Bwana zikubali

Na utakaponiita
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu kweli

Exit mobile version