Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 29 Msingi imara. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 29 Msingi imara. Maneno ya wimbo

 

Msingi imara, enyi wa kweli
Umekwisha pigwa kwa neno hili
Aongeze lipi? mnayo pia
KwaYesu mliomkimbilia

Wambiwapo vuka maji ya giza
Mito ya mashaka taipunguza
Takuwapo nawe, nikuwezeshe
ipate kufaa, isikutishe!

Utakapopishwa ndani ya moto
Nguvu mitakupa, upate pato
Huteketezwi, ila taka zako
Na zitasalia dhahabu zako

Hata zije mvi, walio wangu
Hawaoni kwisha mapenzi yangu
Nazo zitakapowenea, ndipo
Mabegani mwangu niwatwekapo

Na mtu aliyenitegemea
Kamwe kwa adui sitamtia
Nguvu za jehanum zijapotisha
Mtu wangu kamwe sitamuacha

Exit mobile version