Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 27 Baba Yetu aliye Mbinguni. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 27 Baba Yetu aliye Mbinguni. Maneno ya wimbo

 

Baba yetu aliye Mbinguni
Amenifurahisha yakini
Kuniambia mwake Chuoni
Ya kuwa nami Yesu pendoni

Chorus
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda, anipenda
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda mimi

Nimuachapo kutanga mbali
Yeye yu vivyo, hupenda kweli
Hunirejeza kwake moyoni
Kweli yu nami Yesu pendoni

Anipenda! Nami nampenda
Kwa wokovu alionitenda
Akanifia Msalabani
Kwa kuwa namiYesu pendoni

Haya kujua yanipa raha
Kumuamini kuna furaha
Humfukuza mara shetani
Kwona yu nami Yesu pendoni

Sifa ni nyingi asi?wazo
Moja ni sana katika hizo
Wala siachi, hata Mbinguni
Kwimba.“Yu namiYesu pendoni

Exit mobile version