Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 23 Nimekombolewa na Yesu. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 23 Nimekombolewa na Yesu. Maneno ya wimbo

 

Nimekombolewa naYesu
Aliyenirehemia
Kwa bei ya mauti yake
Nimekuwa mtoto wake.

Chorus
Kombolewa!
Nakombolewa na damu
Kombolewa
Mimi mwana wake kweli

Kukombolewa nafurahi
Kupita lugha kutamka
Kulionyesha pendo lake
Nimekuwa mtoto wake

Nitamwona uzuri wake
Mfalme wangu wa ajabu
Na sasa najifurahisha
Katika neema yake

Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu
Muda kitambo atakuja
lli alipo, niwepo

Exit mobile version