Nyimbo Za Sifa
Wimbo 22 Mwokozi Moyoni Mwangu. Maneno ya wimbo
Tangu siku hiyo aliponijia
Akae moyoni mwangu
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu Mwokozi wangu
Chorus
Amani moyoni mwangu
Kwa Yesu, Mwokozi wangu
Sina shaka kamwe
Kwa sababu Yeye
Yu nami moyoni mwangu
Sina haja tena ya kutanga-tanga
Ndiye Kiongozi wangu
Dhambi zangu zote
zimeondolewa
Na Yesu, Mwanawe Mungu
Matumaini yangu ni ya hakika
Katika Mwokozi wangu
Hofu zangu na hamu zimeondoka
Kwa kuwa ninaye Yesu
Siogopi tena nikiitwa kufa
Yu nami daima,Yesu
Mlango wa Mbinguni ni Yeye pia
Tapita humo kwa damu’
Nitaketi na Yeye huko milele
Nisifu Mwokozi wangu
Nina raha moyoni majira yote
Kwa Yesu, Mwanawe Mungu