Nyimbo Za Sifa
Wimbo 21 Ni Salama Rohoni Mwangu. Maneno ya wimbo
Nionapo amani kama shwari
Ama nionapo shida
Kwa mambo yote umenijulisha
Ni safama rohoni mwangu
Chorus
Salama rohoni
Ni salama rohoni mwangu
lngawa shetani atanitesa
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu
Amekufa kwa roho yangu
Dhambi zangu zote, wala si nusu
Zimewekwa Msalabani
Wala sichukui laana yake
Ni salama rohoni mwangu
Ee Bwana himiza siku ya kuja
Panda itakapolia
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu