Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 2 Nilikuwa Kondoo Aliyepotea. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 2 Nilikuwa Kondoo Aliyepotea. Maneno ya wimbo

 

Nilikuwa kondoo aliyepotea
Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea
Nilikuwa mwana asiyesikia
Sikupenda Baba yangu wala kutulia

Na Mchunga Mwema alinitafuta
Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta
Karibu ya kufa kwa kiu na kwa njaa
Waliniona mnyonge, waliniokoa

Yesu ni Mchunga, mwenziwe hapana
Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana
Kwa vidonda vyangu alicia dawa
Ndiye ahyenipata, na kwake nalindwa

Nilikuwa kondoo aliyepotea
Sasa nampenda Baba, na Mchunga pia
Kwanza nilitanga na kukosa sana
Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.

Exit mobile version