Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 2 Mwamba Wenye lmara. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 2 Mwamba Wenye lmara. Maneno ya wimbo

 

Mwamba wenye imara
Kwako nitaji?cha!
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu
Hunisafi na dhambi
Hunifanya mshindi

Kwa kazi zote pia
Sitimizi sharia
Nijapofanya bidii
Nikilia na kudhii
Hayaishi makosa
Ndiwe wa kuokoa

Sina cha mkononi
Naja Msalabani
Nili tupu, nivike
Ni mnyonge, nishike
Nili mchafu naja
Nioshe nisijafa

Nikungojapo chini
Nakwenda kaburini
Nipaapo Mbinguni
Na kukwona enzini
Roho yangu na iwe
Rahani mwako wewe

Exit mobile version