Nyimbo Za Sifa
Wimbo 2 Hata Ndimi Elfu. Maneno ya wimbo
Hata ndimi elfu elfu
Hazitoshi kweli
BwanaYesu kumsifu
Kwa zake fadhili
Yesu, jina liwezalo
Kufukuza hofu;
Lanifurahisha hilo
Lanipa wokovu
jina hili ni uzima
Ni afya; amani;
Laleta habari njema;
Twalipiwa deni
Yesu huvunja mapingu
Ya dhambi moyoni
Msamaha, tena nguvu
Twapata rohoni
Kwa sauti yake vile
Wafu hufufuka
Wakafurahi milele
Pasipo mashaka
Ewe Yesu wangu Bwana
Uwezo nipewe
Kuhubiri kote sana
Wote wakujue