Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 185 Ewe Mchunga Mpole. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 185 Ewe Mchunga Mpole. Maneno ya wimbo

 

Ewe mchunga mpole
Ni pendo zako twajua
Mtoto mpendwa yule
Ulivyomwondoa sasa
Maumivu, la ! hapana
Wala hayaoni tena

Hapa chini duniani
Ni majonzi na mashaka
Yu hali njema mbinguni
Hataona kusumbuka
Huko amekubaliwa
Naye amefurahiwa

Nawe, mwenziwe, ?kiri
Labda mwito ni karibu
Na wewe je, u tayari
Kuitika na kujibu
Kwa furaha,“Bwana niko
Chukua mtoto wako?”

Exit mobile version