Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 181 Lala Rafiki lala Mpenzi. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 181 Lala Rafiki lala Mpenzi. Maneno ya wimbo

 

Lala rafiki, lala mpenzi
Laza kichwa chako kwa Mwokozi
Lala vyema, lala usingizi
Lala, lala vyema

A! mpenzi, sisi twakupenda
Si kama akupendavyo Bwana
Mapenzi yake yazidi sana
Lala, lala vyema

Ulivyolala ni kama mwana
Huamki kwa taabu tena
Raha ndaki utulivu sana
Lala, lala vyema

Hata vivuli vyetu vitoke
Hata nganu ghalani iwekwe
Hata kuche, tupambaukiwe
Lala, lala vyema

Hata jua tukufu litoke
Hata wafu wema wafufuke
Waje na jesu, waume, wake
Lala, lala vyema

Hata ukipambwa kwa mapenzi
Uwe mfano wake Mwokozi
Ukavikwe taji na Mwenyezi
Lala, lala vyema

Siko kuagana, si “Kwa heri”
Punde atakuja atukiri
Uwe umoja kwake wa heri
Lala, lala vyema

Mpaka twonane mbele zake
Na mavazi awapayo wake
Hata ya siri yafunuliwe
Lala, lala vyema

Exit mobile version