Nyimbo Za Sifa
Wimbo 180 Ametwaliwa Rafiki Yetu. Maneno ya wimbo
Ametwaliwa rafiki yetu
Hatutamwona tena mwilini
Ameondolewa huku kwetu
Amezikwa mwili kaburini
Ametwaliwa mwenye kupendwa
Nasi twamlilia machozi
Hako chini tena, ameitwa
Kusimama juu kwa Mwokozi
Ametwaliwa, nasi twajua
Ndivyo alivyotaka Mwenyezi
Ni Bwana aliyemchukua
Ndake furaha, ndetu majonzi
Ametwaliwa, twatumainia
Mwishoni juu tutaonana
Pamoja tutaimba mbinguni
Pamoja tutaketi kwa Bwana