Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 18 Ninaye Rafiki Naye. Maneno ya wimbo

Nyimbo Za Sifa

Wimbo 18 Ninaye Rafiki Naye. Maneno ya wimbo

 

Ninanye Rafiki naye
Alinipenda mbele
Kwa kamba za pendo zake
Nimefungwa milele
Aukaza moyo wangu
Uache mageule
Mimi wake,Yeye wangu
Ndimi naye milele

Ninaye Rafiki ndiye
Aiiyenifilia
Alimwaga damu yake
Kwa watu wote pia
Sina kitu mimi tena
Nikiwa navyo tele
Pia vyote ni amana
Ndimi wake milele

Ninaye Rafiki naye
Uwezo amepewa
Atanilinda mwenyewe
juu tachukuliwa
Nikitazama Mbinguni
Hupata nguvu tele
Sasa natumika chini
Kisha juu milele

Ninaye Rafiki naye
Anao moyo mwema
Ni Mwalimu, Kiongozi
Mlinzi wa daima
Ni nani wa kunitenga
Na Mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga
Ndimi wake milele

Exit mobile version