Nyimbo Za Sifa
Wimbo 178 Mungu U mapenzi Makamilifu. Maneno ya wimbo
Mungu U mapenzi makamilifu
Yapitayo fahamu za watu
Twanyenyekea sisi wapungufu
Wape baraka wapenzi wetu
Ewe Mapenzi yasiyopimika
Twawaombea kitini mwako
Wape mapenzi yasiyotindika
Waliooana mbele yako
Ewe Uhai,Wewe U dhamana
Ya imani na matumaini
Wape kuvumilia hapa sana
Wasiche maumivu mwishoni
Wape furaha hiyo iwezayo
Kutia nuru kwenye huzuni
Wape amani hiyo itakwayo
Katika matata duniani
Waende mbele kusaidiana
Maisha yao ulimwenguni
Hata mwisho, ni kuja kwake Bwana
Wafurahi milele mbinguni